
Bhasi baada ya shangwe zile mara gafla nikashangaa Niko seblen na Mzee habibu yuko pemben yangu akinambia sasa wewe ni mtu mwingine kabisa katika hii dunia na utamiliki chochote utakacho na utafanya lolote utakalo Hakuna wakukuzuia. Nilibaki Nikiwa siamin maneno ya Mzee habibu lakini kutokana na vimbwanga vya dakika chache zilizopita akili ilianza kukubaliana lakin Bado nilisubiri kuona kwa vitendo. Basi Mzee habibu aliendelea na maneno yake kisha akanikumbusha nisisahau kuhusu ahadi niliyoweka kule kuhusu kutoa kafara na pia siku nzuri ya kutoa kafara ni siku ya sita katika week nayo ni alhamis. Nlimwambia kuwa Siwezi kusahau na kwa hakika Nilikua na chachu ya kufanya hiyo kafara haraka ili nione mafanikio yangu ya kimaisha yakianza. bhasi siku zilisogea na kwa hakika siku ya alhamisi iliwadia na Mzee habibu alinikumbushushia kuwa ndio siku fasaha ya mie kutoa kafara nzuri kwa Mkuu na mie nikaitikia na ilipofika majira ya saa 9 usiku Mzee habibu kwa kuwa alielewa mie Bado sijawa mzoefu Alikuja kuniamsha na kunichukua tukaenda barabara kuu ya magari ya mikoan nako kulikuwa na malori tu yakipita sambamba na magari ya watu binafsi wakitoka katika starehe . Mzee habibu akanambia sasa Ndo muda fasaha wa kutoa kwa ajili ya Mkuu amuru gari lile kugongana na lile kwa jina la Mkuu, mie Nikiwa kama Siamini kama uwezo huo ninao lakin tokana na Mzee habibu alivyonikazia uso Ni kasimama katikati ya ile barabara na kuliamuru Lori moja ligongane na gari dogo kwa nguvu na uwezo wa mkuu wa wakuu na cha ajabu kwel lile gari dogo likaingia uvunguni mwa Lori na kisha yote yakadondoka na kuanza kuburuzika na mwishoe kuwaka moto maana Lori lile lilikua la mafuta. Mzee habibu alinipigia makofi na kusema sasa umekua shujaa na tegemea maajabu makubwa maishani. Kisha akaniambia tiar umetekeleza moja ya ahadi kubwa kwa Mkuu ya kutoa kafara lakin pale umeuwa watano lakini kwa bahati mbaya wote wanaume na unahitajika utoe kafara ya wanaume wawili na mwanamke mmoja. Kwahiyo unadeni la kafara moja ya jinsia ya kike nayo tuelekee kwenye madanguro, basi moja kwa moja tukaelekea mpaka kwenye mtaa ambao Ulikua ukisifika kwa wanawake wanaojiuza na kukuta wanawake wachache tu kwani muda Ulikua umeenda saaana. Basi wale wanawake wakamkimbilia Mzee habibu na kuniacha mie wakiona ni mdogo Siwezi Fanya kitu. Basi Mzee habibu akachagua msichana mmoja mzuri saana kisha akanambia tuondoke na kuelekea sehemu za guest house na kuagiza chumba kisha tukaingia wote ndani ya kile chumba. Mzee habibu aliniita tukaingia bafuni na kuniambia muda wangu kutekeleza moja ya kafara ya mwisho na hii naweza kuifanya nipendavyo iwe kwa kuzungumza au kwa kumkiss au hata kwa kufanyanae Mapenzi ila cha muhimu ni kusema maneno kuwa natenda hili kwa uwezo na nguvu za Mkuu wa Wakuu. Kwa kuwa nilikuwa katika umri wa ukuaji na homoni zilikuwa zikinisumbua basi nilijikuta nikitaman kufanya na yule mtu Mapenzi maana siku wahi kufanya hata mara moja basi niliona hii Ndo nafasi yangu ya pekee kuitumia kujua utamu wa Mapenzi.Nlimwambia Mzee habibu hamna tatizo nitatekeleza kama alivyonielekeza kisha nilirudi alipo yule msichana na kumsogelea na kuanza kumshika shika yule msichana akaniambia hela yangu kwanza vingine Ndo vitafwata kisha akawa anatoa maelekezo ya jinsi ya huduma zake na bei yake . kisha akasema kama mtanitumia wote Wawili bei itakua mara mbili ya hiyo aliyonitajia, nilibaki nikicheka na kumwambia hata ungesema mara tano tungekulipa. Mzee habibu akatoa burunguti la fedha na kumpatia yule msichana lakini kwa fedha zile yule msichana aliogopa saaana na kuhisi tutakuwa sio watu wema na kusema sitaki tena Naomba kuondoka. Mzee habibu akaanza kucheka na kuniambia Hakuna muda wa kupoteza maana kashatia wasiwasi na mie nikatamka yale maneno kisha Mzee habibu akanishika mkono na kupotea eneo lile na kumuacha dada yule akiwa amekaukaa kama mtu alieungua na moto. Basi tulitokea seblen kwa Mzee habibu na kisha Mzee habibu alinipongeza kwa kukamilisha zoez langu la kutoa kafara na kuniambia kafara huwa inatolewa kila baada ya miez 6 katika siku ya sita. Nkamwambia sawa nimemuelewa na nitakuwa nikitekeleza, siku zilisogea na nkaanza kuona mabadiliko haswa katika masomo yangu na maisha kwa ujumla kwani nilikuwa kipenzi cha watu na watu Wengi walipenda saaana ukaribu na mie. Maisha yalisonga na hatimae miaka nayo ikasogea nkamaliza chuo na kuweza kufungua kampuni yangu kubwa ya utengenezaji wa nguo ambazo zote zilikuwa hapa kifuani zinanembo ya sura ya Mkuu. Kwa hakika maisha yaliniendea vizuri na kuwa tajiri Mkubwa saaana lakini wa Mali za kichawi, Mzee habibu umri wake ulikwenda na hatimae muda wake wa kumtumikia Mkuu ulikwisha na Mkuu kuamua kumtoa sadaka.
#itaendeleaaa
No comments